Posts

Showing posts from December, 2017

MAMBO YA KUMSAIDIA KIJANA ALIYEOKOKA AISHI MAISHA YENYE USHUHUDA MZURI

Image
Mtume Paulo katika waraka wake kwa Timotheo anamwambia hivi, ‘Mtu awaye yote  ASIUDHARAU  ujana wako, bali uwe  KIELELEZO  kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.  JITUNZE  nafsi yako, na mafundisho yako.  DUMU  katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo  UTAJIOKOA NAFSI YAKO NA WALE WAKUSIKIAO PIA’  (1Timotheo 4:12 & 14). Sentensi hizi zinatuonyesha kwamba kijana yeyote ambaye amefanya uamuzi wa kuokoka, kwa hakika amefanya maamuzi ambayo yanamtaka amaanishe katika kumfuata kwake Yesu au kuuishi wakovu wake. Pamoja na kumpa Yesu maisha yake ni lazima kijana afanye maamuzi ya kuishi maisha ya kudumu kumpendeza Mungu kwa kuzikubali gharama zinazohusiana na wokovu aliouchagua na si kuishi maisha yenye kupelekea jina la BWANA kutukanwa kama ilivyo kwa baadhi ya vijana wengi leo. Ukisoma mstari huu wa 1Timotheo 4:14 kwenye toleo la kiingereza la ESV unasema  ‘ Keep a close watch on yoursel...

MFAHAMU ROHO MTAKATIFU VIZURI ILI UPATE MSAADA KATIKA NJIA ZAKO ZOTE

Image
nilitamani tuzungumze habari za Roho Mtakatifu kwa undani tuangalie vitabu vinavyoelezea Roho Mtakatifu katika biblia tuangalie watu waliowahi kujazwa roho Mtakatifu. Na kutembea na Roho Mtakatifu. Jinsi ya kusikia Roho Mtakatifu. Je unajua kikanuni unaweza kuomba ujazo Roho Mtakatifu ukajazwa hata chumbani kwako? Hasara za kutoongozwa na Roho Mtakatifu! Faida za Roho Mtakatifu. Wangapi wangependa tushirikiane? Kuna vitu viwili vinavyofanya wakristo washindwe vita moja kutokutumia damu ya Yesu kwa usahihi, ya pili, kuomba bila roho Mtakatifu kumpa roho Mtakatifu asilimia chache ya maisha . #Tuangalie kwanini kanisa la sasa linaomba sana kuliko kanisa la zamani. Lakini sasa hakuna matokeo makubwa kama ya zamani! What is the different? Wao walikuwa na Roho Mtakatifu na sisi tunaye! Inakuwaje kuwaje? hayo ni mambo ya kuyangalia. Jinsi unavyojifunza habari za Roho Mtakatifu ndivyo jinsi unamvutia aje kwako! Ndivyo jinsi atajifunua kwako zaidi. # Kitabu cha Matendo ya mitume kimeelezea haba...

JINSI YA KUKUA KIROHO

Image
Utaendelea vizuri katika maisha ya kiroho ukiyafuata mashauri yafuatayo kila siku: 1;Zungumza na MUNGU kwa maombi (Yohana 15:7) Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. 2: Soma Neno la MUNGU (Matendo 17:11) Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo. 3;Uwe mwaminifu kwa MUNGU (Yohana 14:21) Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake. 4;Mshuhudie KRISTO kwa matendo yako na maneno yako (Mathayo 4:19Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu. naYohana 15:8) Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu. 5; Umtumaini MUNGU kwa kila jambo katika maisha yako (1 Petro 5:7) huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha san...