JINSI YA KUKUA KIROHO

Utaendelea vizuri katika maisha ya kiroho ukiyafuata mashauri yafuatayo kila siku:

1;Zungumza na MUNGU kwa maombi (Yohana 15:7)
Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.
2: Soma Neno la MUNGU (Matendo 17:11)
Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.
3;Uwe mwaminifu kwa MUNGU (Yohana 14:21)
Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.
4;Mshuhudie KRISTO kwa matendo yako na maneno yako (Mathayo 4:19Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu. naYohana 15:8)
Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.
5; Umtumaini MUNGU kwa kila jambo katika maisha yako (1 Petro 5:7)
huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.
6: Umruhusu ROHO MTAKATIFU akutawale (Wagalatia 5:16-18Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria. na Matendo 1:8)Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.

Comments

Popular posts from this blog

MFAHAMU ROHO MTAKATIFU VIZURI ILI UPATE MSAADA KATIKA NJIA ZAKO ZOTE

MAMBO YA KUMSAIDIA KIJANA ALIYEOKOKA AISHI MAISHA YENYE USHUHUDA MZURI